Thursday, 13 January 2011

ONYO:- KAMA MUOGA USIANGALIE .......! Laparoscopic Cholecystectomy - Michael Bickford, FRACS



http://www.youtube.com/watch?v=fz48sITkdJ0&NR=1

Nina DVD ya procedure yangu lakini kwa sababu za kimaadili nawawekea hii ili pia mpate na elimu kidogo.
Hii ndio procedure (sijui kwa kiswahili ni nini- Hatua, mwenendo?) ambayo nimeipitia, yaani ni sawa kabisa na yangu.

Usilolijua Litakusumbua kama usiku wa giza nene



Wandugu wapendwa, Natumai kwa kudra za mwenyezi Mungu mmesalimika wote. Heri ya mwaka mpya kwenu wote.

Nashukuru kuuona huu mwaka nikiwa mzima, kwani mwaka uliopita ulikuwa mgumu sana kwangu kwani niliugua hadi nikafikiri sitaumaliza mwaka 2010. Kuna siku niliugua sana na madaktari walihangaika sana lakini wakawa hawafanikiwi kiasi kwamba wakabaki wamenitazama tu wasijue la kufanya kwani nilikuwa nimeshachomwa sindano kadhaa na drip kadhaa na vidonge ndio usiseme hivyo wakahofia wangeweza kunipoteza kwa kunioverdose. Nilipoona madaktari kama wameshindwa nikatokwa na chozi la uchungu nikajua masikini mimi ndio nawaacha wanangu na (mume wangu ofkoz)Nikamuita mume wangu na kumwambia aniitie ndugu yangu ambaye pia ni rafiki yangu (Irene) ili nimkabidhi watoto lol!!!! (siyo utani)Lakini naye akabaki ananiangalia asijue la kufanya. Ukweli ni kwamba nimeugua kwa takribani miaka miwili nikijua ni vidonda vya tumbo yaani "ulcers" na nimekuwa naishi maisha ya ki-ulcers (sijui kama mnanielewa hapa) yaani kila dakika nina dawa tena dawa kweli maana kila nikienda hospitali nabadilishiwa dawa kuwa kama hizi hazikufaa basi tumia hizi amabazo ni strong zaidi basi namimi nabugia tu. Jamani hata vyakula yaani limitation zilikuwa kibao, cha kushangaza hata nikifuata masharti ilikuwa kuna siku zalipuka nakwambia tena mara nyingi ilikuwa ni usiku wa manane basi mbio hospitali na nikifika kule nadungwa masindano immediately napona narudi home, kwa hiyo nikawa nimeridhika kwamba haya ndio maisha yangu na hayo masindano ndio pona yangu. Sasa toka Oktoba ndio mambo yakawa mabay ikawa hayo masindano hayafai tena maumivu ni makali balaa. Hiyo siku ambayo madkatari walibaki wananitolea macho ndio wakashauri nifanye tena vipimo ili kujua hali imekuwa mbaya kiasi gani, lohh!!! haki walikuta kama ulcers ziliwahi kuwepo basi zimepona muda mrefu sana isipokuwa nilikuwa na Kidney stones na gall stone tobaaa!!! Gall stone zimefanya kifuko cha nyongo kuvimba na ile ngozi ya mfuko wa nyongo kuwa thick na mbaya zaidi (kwa maana ya hatari) ni kwamba kulikuwa na mawe makubwa 7 na madogo mengi yasiyo na idadi na kati ya hayo madogo kuna moja linastrugle kupenetrate kuingia kwenye one of the tube inayopeleka bile kwenye system na kama ingefanikiwa basi ingekuwa tragedy kwani madhara yake yangekuwa makubwa mno. Daktari akashauri urgent operation.... loh nilikuwa mdogo kama nukta (.)nikifikiria kisu kwa tumbo langu nilikuwa sijielewi halafu nikawaza mikasi itakavyoachwa tumboni sikupata jibu na je wangenipasaua kichwa badala ya tumbo duh....!!! Nilikuwa sipati jibu (ukizingatia ni urgent operation) Nikapiga moyo konde nikaona bora nipige moyo konde niende nchi za wenzetu ambao wanajitahidi kuzuwia majanga yasiyokuwa ya lazima. Nikaenda nikafanyiwa procedure inaitwa Laparascopic ni procedure nzuri na haisumbui sana wanachofanya ni kuweka matundu madogo madogo kama manne then wakatoa kifuko chote cha nyongo. Hapa nilipo ni mzima nyuzi zilishatoka na kazi nimeanza nina siku 3 kazini. Namshukuru Mungu kwa kunisaidia kugundua tatizo kabla mambo hayajaharibika, kwani kama kile kijiwe kingepita kwenye ule mrija basi kingeziba na matokeo yake nyongo ingemwagika kwenye ini nami ningekuwa wa njano na kunisaidia baada ya hapo ingekuwa ni kwa miujiza ya Mungu!!!!



Eti nijuzeni madhara ya kutoa kifuko cha nyongo ni nini?

Wapendwa nimerudi tena naomba mnipokee na tushirikiane kama zamani!!!