Showing posts with label Ng'wanambiti. Show all posts
Showing posts with label Ng'wanambiti. Show all posts

Thursday, 8 July 2010

Ugeni Mzito


Amani iwe kwenu.
Leo nimepata ugeni mzito sana toka kanda ya Ziwa - Musoma
Nimeshangaa sana halafu nikafurahi sana kumpata mgeni huyu ambaye nahisi yupo mbioni kutangaza nia!!!

Alifika asubuhi sana ofisini kwangu na kufanikiwa kunibamba kuwa ni mchelewaji ofisini.

Chacha "Ng'wanambiti" nimefurahia sana ujio wako, nakutakia safari njema na ukaribie tena utakapokuja jijini. Fanya hima utukutanishe bloggers wenzako ambao tunajitia busy kupambana na mafoleni maana huku kwetu twatoka alfajiri na kurudi usiku mwingi kiasi kwamba hatuna hata muda wa kufahamiana na watu wapya maishani.

Hivi vijisimu vya kichina vinasaidia japo kwaliti ya picha si nzuri sana lakini si haba.