Thursday 8 July 2010

Ugeni Mzito


Amani iwe kwenu.
Leo nimepata ugeni mzito sana toka kanda ya Ziwa - Musoma
Nimeshangaa sana halafu nikafurahi sana kumpata mgeni huyu ambaye nahisi yupo mbioni kutangaza nia!!!

Alifika asubuhi sana ofisini kwangu na kufanikiwa kunibamba kuwa ni mchelewaji ofisini.

Chacha "Ng'wanambiti" nimefurahia sana ujio wako, nakutakia safari njema na ukaribie tena utakapokuja jijini. Fanya hima utukutanishe bloggers wenzako ambao tunajitia busy kupambana na mafoleni maana huku kwetu twatoka alfajiri na kurudi usiku mwingi kiasi kwamba hatuna hata muda wa kufahamiana na watu wapya maishani.

Hivi vijisimu vya kichina vinasaidia japo kwaliti ya picha si nzuri sana lakini si haba.

5 comments:

  1. Wow! Kwa kweli ni bahati sana kukutana na watu ambao mmejuana mtandaoni au niseme ka bloggers. Kwa kweli inafurahisha sana naona mwanzo ni mzuri pia nawaonea wivu wote mnaokutana sijui kwa nini mimi sikutani na mtu hata mmoja nijapo nyumbani? mmmhhh!!

    ReplyDelete
  2. Nasikitika kwamba sikualikwa kwenye mkutano huo wa ghafla, ingawa mliniringishia kwa njia ya simu.
    Naamini huo ni mwanzo mzuri na kunapo majaaliwa kukutana kwenu kunaweza kukawa ni ishara ya kuwakutanisha wanablog woote hapa nchini........yaweza kuwa ndoto za Alinacha!?

    ReplyDelete
  3. Nimerudi tena. Nilisahau kusema neno ya kwamba mmependeza kweli kama.....lol kapulya mimi. kaka Kaluse unasema kweli:- nanukuu "Naamini huo ni mwanzo mzuri na kunapo majaaliwa kukutana kwenu kunaweza kukawa ni ishara ya kuwakutanisha wanablog woote hapa nchini........yaweza kuwa ndoto za Alinacha!?"

    ReplyDelete
  4. Yasinta masihara hayo acha kabisa unajua kuwa Ng'wanambiti ni Mkatoliki mwenye siasa kali aka Paroko. Kaluse pole hatukukualika kwani tulikaa kama tume maalum ya kuangalia uwezekano wa kuwakutanisha wanablog next week pale movin pick. Yasinta tualike wanablog tuje tukutembelee huko au unataka sisi tukualike uje huku?

    ReplyDelete
  5. Da`karibuni sana na kwanza hamhitaji mwaliko. Pia mnaweza kunialika. Ha ha ha Eti niache masihara....habari ndio hiyo:-)

    ReplyDelete