Friday 9 July 2010

Weekend hiyoo. Je ya kwako itakuwaje?

Mipango yangu ya weekend hii ni kama hivi:
Namaliza kazi saa nane, saa nane na nusu naenda kulaunch a new beauty palour in Masaki nitawapa post zake na contacts kwa wale watakaopenda kwenda au kupeleka vidosho wao. Saa kumi nina kikao cha send off na kitchen party. nikimaliza hapo huyoo naenda zangu viwanja vya Mzalendo (jamani mateso haya) yaani mtu hupumziki lol!!! Kesho naenda Morogoro kumpeleka mtoto shule st. Anne girls seminary. Jumapili asubuhi church, mchana kupeleka watoto kucheza jioni salon na weekend inakuwa imeisha. I wish weekend ingekuwa siku nne kwa week.

5 comments:

  1. Naona umeplane mwisho wa juma hili maana mmh. Binafsi nimemaliza kazi saa sita mchan huu na nimerudi nyumbani na nimepata chakula cha mcha na kisha napumzika, kesho na kesho kutwa nitakuwa napumzika tu hakuna kazi nitakuwa na familia yangu labda kutembela beach:-) mwisho wa juma mwema kwako pia dadangu!!

    ReplyDelete
  2. Weee Lulu weee! Umekuwa roboti? kazi zote mtu mmoja? Niajiri nkusaidie baadhi!!!

    Mie nimeumwa na NGE hivo niko home nimejilalia tu! Sina mpango na outing kabsaa!

    Halafu naona bado uko utumwani kwa kuhusudu mambo ya chiken na sendingi-ofu ntakusemea!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Yasinta natamani ningeweza kukaa na watoto nyumbani ila huku home vurugu usipotokea kwenye issue za watu kama vikao n.k.

    Chacha nge kakung'ata sehemu gani ya mwili?

    ReplyDelete
  5. Aisee, kwa mara ya kwanza ktk maisha yangu nimeng'atwa na nge mguu wa kulia. Maumivu mpaka ikulu! Wooooi!

    ReplyDelete